WATANGAZAJI wa Clouds Media, SoudyBrown, Shaffih Dauda, msanii Maua Sama, mpigapicha, MX, mshereheshaji MC Luvanda na watuhumiwa wengine wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 24, 2018, kwa ajili kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Washitakiwa hao walishuka kwenye karandinga la polisi wakitokea Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam walikokuwa wameshikiliwa huku wakiwa wamevalia kininja ili kuficha nyuso zao.
Soudy Brown na Maua Sama wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za udhalilishaji wa nembo ya taifa baada ya kusambaa clips za video zinazowaonyesha watu wakichezea pesa halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Watuhumiwa wengine wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kuchapisha maudhui kwenye mitandao ya kijamii wanayomiliki (Blogs na YouTube) bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano  nchini (TCRA).

Ombi lao la kupata dhamana linatarajiwa kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi.

SHUHUDIA SOUDY NA WENZAKE WALIVYOTINGA KININJA