Navy Kenzo
BAADA ya kusemwa kila kona kuwa wamehamia Wasafi Classic Baby (WCB), msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Aika Marealle ‘Aika’ ameanika undani kuwa hayupo WCB bali yupo chini ya meneja Sallam Shariff ‘Sallam SK’ ambaye anawasimamia kimuziki.
Akizungumza na Showbiz Xtra, Aika anayeunda kundi moja la Navy Kenzo akiwa na mpenzi wake, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ alisema kuwa, amekuwa akisikia kwa watu wengi juu ya kuhamia WCB mara baada ya kuachia wimbo wao wa Katika waliomshirikisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ jambo ambalo halina ukweli.“Yaani watu wengi wanasema nimehamia WCB lakini ukweli ni kwamba tuna meneja anayetokea huko anaitwa Sallam na amekuwa akitusimamia sasa sijui hayo mengine yanatokea wapi. “Nilikaa na mwenzangu tukatunga Wimbo wa Katika tukaona ni vizuri tukamshirikisha Diamond ndiyo ikawa hivyo sasa nashangaa hao wanaoungaunga maneno,” alisema Aika.
STORI: NEEMA ADRIAN