Kompany alijikita katika siasa akiwa diwani tangu mwaka 2006, na baadaye kupata ubunge katika jimbo moja jijini Brussels mwaka 2014. Lakini huenda umaarufu wake unatokana na mwanaye ambaye ni mchezaji na nahodha wa klabu ya Manchester City ya Uingereza iliyoko kwenye ligi kuu ya nchi hiyo, na pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ubelgji.
Kaka yake Vincent aitwaye, Francois, naye hucheza soka na klabu ya KSV Roeselare ya Ubelgiji.
“Baba yangu ni meya wa kwanza mwesi wa Ubelgiji, haijawahi kutokea katika historia, hongera baba yangu!” aliandika Vincent kwenye akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram.
0 Comments