TAKRIBANI watu kumi wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya New Force lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam kutumbukia katika mteremko wa Mlima Kitonga mkoani Iringa.


Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni basi hilo kupoteza mwelekeo wakati lilipokuwa likipishana na gari dogo katika eneo la mlima huo.

“Hali za majeruhi wanaendelea vizuri, na wamefikishwa kwenye kituo cha afya cha serikali kwaajili ya uangalizi na kupatiwa vipimo zaidi”, amesema Kasesela.

Amesema kuwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani anaelekea eneo la tukio muda huu, endelea kufuatilia taarifa zetu.