Msemaji wa Simba, Haji Manara.
MSEMAJI  wa Klabu ya Simba, Haji Manara, ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa takribani siku nne.
Manara alishikiliwa kwa mahojiano siku moja tu baada ya kutekwa kwa mwanachama mwekezaji maarufu wa Simba, Mohamed Dewji.
Dewji maarufu kama Mo, alitekwa na watu wasiojulikana wakielezwa ni raia wa kigeni akiwa anaingia gym ya mazoezi kwenye Hoteli ya Collosseum eneo la Oyster Bay jijini Dar es Salaam, alfajiri ya Alhamisi iliyopita.