Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son, akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za makao makuu ya Halotel wakati wa hafla fupi ya kusherekea maadhimisho ya miaka mitatu ya kampuni hiyo kutoa huduma za mawasiliano Tanzania tangu ilipozinduliwa nchini mwaka 2015. (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Kampuni hiyo Mhina Semwenda.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari, katika ofisi za makao makuu ya Halotel ambapo akielezea mafanikio waliyoyapata kwa kuwafikishia huduma za mawasiliano wananchi waliopo vijijini ndani ya miaka mitatu ya utoaji huduma. wakati wa hafla fupi ya kusherekea maadhimisho ya miaka mitatu ya kampuni hiyo, Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son na katibu wa kampuni hiyo Nguyen Thi Thuy Linh
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda, akijibu maswali ya wanahabari wakati alipozungumza nao katika ofisi za makao makuu ya Halotel ambapo ameelezea mafanikio waliyoyapata kwa kuwafikishia huduma za mawasiliano wananchi waliopo vijijini ndani ya miaka mitatu ya utoaji huduma. wakati wa hafla fupi ya kusherekea maadhimisho ya miaka mitatu ya kampuni hiyo, Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari, katika ofisi za makao makuu ya Halotel ambapo akielezea mafanikio waliyoyapata kwa kuwafikishia huduma za mawasiliano wananchi waliopo vijijini ndani ya miaka mitatu ya utoaji huduma. wakati wa hafla fupi ya kusherekea maadhimisho ya miaka mitatu ya kampuni hiyo, Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son na kushoto katibu wa kampuni hiyo Nguyen Thi Thuy Linh


Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Tanzania inaadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa huduma za Kampuni hiyo ya mtandao wa simu za mkononi hapa nchini. 

Hayo yamezungumzwa na Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Bw. Nguyen Van Son wakati akizungumza na waandishi wa habri kuhusu siku hii ili kuonyesha mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Kampuni hiyo kwa kipindi chote tangu ilipoanza kutoa huduma hapa nchini 

Nguyen Van Son amesema kuna mikakati mipya kuanzia sasa ambapo Halotel Tanzania inakusudia kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani Milioni 700 katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania ikiwa na malengo ya kuwa nafasi ya pili na kuwafikia wateja zaidi ya Milioni 6 katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza.

Pamoja na mipango hiyo , Halotel Tanania imekusudia kuendelea kuiboresha huduma ya utumaji wa pesa kwa njia ya Mtandao ijulikanayo kama ‘Halopesa’ sambamba na kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ‘ICT’ kwa ajili ya wateja wa Mashirika Binafsi na Serikali kwa ujumla.

Ameongeza kuwa “Katika kipindi cha miaka mitatu tunapoadhimisha siku hii, Halotel Tanzania tayari imefanya uwekezaji unaofikia Dola za Marekani Milioni 500, ikiwa ndiyo kampuni inayoongoza kwa kuwekeza miundombinu ya Mawasiliano sehemu mbalimbali nchini inayowafikia asilimia 95 ya wananchi wote ikiwa na vituo 4,400 vya kupokea mawasioliano (BTS’s) kwa umbali wa Kilomita 18,300”.

Bw.Nguyen Van Son ameongeza kuwa mpango wa biashara wa Halotel zaidi umelenga kuwafikia watu walioko pembezoni mwa miji kwa kuwapa gharama nafuu za mawasiliano huku ikiwa tayari imewafikia wananchi zaidi ya Milioni tatu sambamba na Milioni moja wengine waliojiunga na mtandao wa Halopesa

Hivi karibuni pia Halotel Tanzania itawekeza kiasi cha Dola za Marekani Milioni 200 kwa ajili ya kuboresha huduma za mtandao na zaidi kuhakikisha inaimarisha mtandao wa 4G kwa wateja wake kote nchini.Amesongeza kuwa Kampuni hiyo itaboresha huduma zake mbalimbali ikiwa na lengo la kuwafikia wateja zaidi ya Milioni 6 pamoja na watumiaji Milioni 3 wa huduma ya Halopesa baada ya miaka mitano kuanzia mwaka ujao , pamoja na kuboresha huduma kwa wateja wake wakubwa kutoka Taasisi mbalimbali za kibiashara za Binafsi na Serikali.

Kampuni hiyo inaamini kuwa kupitia huduma hizi itakuwa tumeisaidia Serikali na taasisi zote za kibiashara kuendeleza utoaji wa huduma kwa ufanisi wakati huu ambao pia inatarajia kuandaa mfumo maalumu kwa wateja wake utakaowawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi.Kupitia mikakati mbalimbali ya Kampuni hiyo, itaweza kufikia lengo la kuwa kampuni namba mbili inayotoa Mawasiliano yenye tija hapa nchini.

Mbali na hiyo Halotel imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii inayoliwezesha Taifa kufikia malengo yake mbalimbali