Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema mwaka jana katika mbio za Mwenge kuna miradi ilizinduliwa lakini katika mbio za mwaka huu 2018 miradi hiyo ilipokaguliwa haijaonekana likiwemo duka la dawa za binadamu lililozinduliwa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu.


Magufuli ametoa maagizo hayo leo Oktoba 15 akiwa Ikulu jijini Dar alipokutana na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu na kuzungumza nao.

“Kwa utaratibu waliouweka mwaka huu, wakimbiza mwenge waliipitia tena baadhi ya miradi kuicheki tena kama bado ipo, imegundulika kuna miradi mitano ambayo haipo, ilizinduliwa mwaka jana 2017 lakini wamepita mwaka huu haipo, miongoni mwa miradi hiyo ni duka la madawa Bariadi.

“Kwenye hili nataka wakuu wa wilaya na wa mikoa wajieleze vizuri, hii maana yake hawasimamii hiyo miradi iliyozinduliwa, lilipofunguliwa hilo duka kulikuwa na madawa yote, waliporudi mwaka huu hakuna kitu, kwa hiyo ilikuwa ni kama shoo,” alisema Magufuli.

Aidha, amesema kutoonekana kwa miradi hiyo ni kuudanganya Mwenge na kumdanganya Baba wa Taifa ambaye ni Mwanzilishi na kiini wa Mwenge wa Taifa.

Wakimbiza Mwenge aliongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.

BREAKING: Je Rais Magufuli ‘atawatumbua’ ma DC hawa?