ALIYEKUWA Katibu wa Yanga, Boni¬face Mkwasa, anatarajia ku¬rudi India kwa mara nyingine tena Novemba 6 kwa ajili ya ku¬fanyiwa vipimo huku akifunguka kuwa anaendelea vizuri.

Mkwasa alifany¬iwa upasuaji wa moyo mwanzoni mwa Agosti, mwa¬ka huu, baada ya kujiuzulu nafasi yake ya ukatibu Yanga kutokana na sababu za kiafya na nafasi yake kukaimiwa na Omary Kaya.
Akizungumza na Championi Ju¬matatu, Mkwasa alisema kuwa anaen¬delea vizuri kiafya kwani amezingatia masharti yote aliy¬opewa na dokta wake ila ana¬tarajia kwenda India tena kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
“Kwa sasa ninaendelea vizuri na hali yangu imezidi kuimarika kwani nazingatia masharti yote niliyopewa na dokta lakini pia na¬hudhuria kliniki kwa dokta Lwakatare ila natarajia kwenda India tena kwa ajili ya kufanyiwa check up katika hospitali ile ya mwanzo lakini kuhusu kurejea Yanga nitaan¬galia baada ya miezi sita kupita,” alisema Mkwasa.
Ibrahim Mressy, Dar es Salaam