Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akikagua eneo linalotumika kuuza nyama ya Ng`ombe na Mbuzi.


 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  akizungumza na wananchi
(wadau) wa machinjio ya Vingunguti  kuhusu kero zao mbalimbali
wazipatazo kuhusu eneo hilo la Mchinjio.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  akizungumza na
wananchi(wadau) wa machinjio ya Vingunguti ambapo amewahakikishi
serikali ya awamu ya tano ipo pamoja nao na amewaomba kulipa kodi ili
kuinua uchumi wa Taifa.


 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto
akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
jana  katika machinjio ya vingunguti  jijini Dar es Salaam.


 Wadau wa machinjio ya Vingunguti wakiendelea na kazi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Na Mwandishi Wetu,Globu ya jamii

SHILINGI
bilioni tatu zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa  machinjio ya Vingunguti
jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi unatarajia kuanza  Novemba mwaka
huu.


Uamuzi wa kutengwa kwa fedha hizo ni katika jitihada za kuondoa changamoto zinazoikabili machinjio hayo.

Hayo
ameelezwa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini
Dar es Salaam  mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega.


Ulega
alifanya ziara fupi katika machinjio hiyo akiambata na viongozi wengine
wa serikali wakiwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Ilala, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Nyama, Dk wa Mifugo na Mkurugenzi
Msaidizi wa  Masoko na uzalishaji toka Wizarani.


Katika
ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega alielezwa changamoto zinazoikabili
machinjio hiyo ikiwa ni pamoja na  wafanyabiashara wa nyama kutozwa
ushuru mkubwa kwa mazao ya mifugo, ukosekanaji wa  soko la uhakika la
ngozi, ambapo Ulega amesema Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya
Mifugo na Uvuvi ina mkakati  kabambe wa kukabiliana na changamoto hizo.


Ulega amefafanua  kwa kuanza na ujenzi wa machinjio mpya ya kisasa utakaofanyika kwa gharama hizo za fedha za Serikali.

“Wasimamizi
wote wa ujenzi wa machinjio hii  nawataka muhakikishe kuwa ujenzi huu
unafanyika kwa haraka na ubora ili machinjio hii iweze kuchinja ng’ombe,
mbuzi, kondoo na kuku kwa kuwa machinjio nyingi zilizojengwa
hazijazingatia suala la uchinjaji wa kuku,” amesisitiza Ulega.


 Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(katikati)  akiwasili kwenye
eneo la machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili wadau wa machinjio hayo jana jijini  Dar es Salaam.(Picha
na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)