Pichani kati Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Ruty akirudishwa rumande huku upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Wakati Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Ruty na mpenzi wake Said Kitomali wakiendelea kusota rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile upelekezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Amber Ruty na Said wanashtakiwa pamoja na James Charles maarufu kama 'James Delicious' ambaye yeye yupo nje kwa dhamana.kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwizile kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika.

Hata hivyo, Hakimu Rwizile  amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa.Kesi  hiyo imeahirisha hadi Decemba 10,2018.

Katika kesi hiyo, Amber Ruth,  anadaiwa kufanya mapenzi kinyume na maumbil kosa analodaiwa kulitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, 


Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Ruth kinyume na maumbile.Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.


Katika shtaka la nne ambalo ni kusababisha kusambaa kwa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati ya 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.Amber  Rutty na mpenzi wake ili waweze kuwa nje kwa dhamana wanatakiwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 15.


Pia wadhamini wawe na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zenu za kusafiria na msitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.