Calissah (wa nne kushoto) akiwa na washindani wenzake.
Mwanamitindo wa kiume Tanzania, Callisah ameibuka mshindi wa Mister Africa International 2018 katika mashindano yaliyofanyika nchini Nigeria.


Shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Lagos, Nigeria na kushirikisha nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo Lesotho, Nigeria, Ghana, Cameroon na nyingine.

Kupitia akaunti ya Instagram ya Mister Africa International, Calisa alitangazwa kushika nafasi ya kwanza. 
Calisa katika akaunti yake ya instagram ameandika, “Hii sio yangu, ni yetu. Thank you Tanzania, thank you East Africa,thank you Africa. Asante kwa wote walionisapoti kwenye kila hatua ya kufanikisha hili”.