Taarifa ya Shirika la Ndege la Ethiopia imesema kuwa abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege ya shirika hilo iliyopata ajali wote wamefariki.
Msemaji wa kampuni hiyo, Asrat Begashaw, amesema ndege ya kampuni hiyo aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Addis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi.

Mkurugenzi Mkuu wa Ethiopian Airlines akiwa katika eneo la tukio la ajali.
Taarifa hiyo imefafanua kwamba walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole mjini Addis Ababa.
Msemaji huyo alisema wasafiri 149 na wahudumu wanane waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hakuna hata mmoja aliyenusurika, wote wamekufa, aliliambia Shirika la Habari la Kitaifa la Ethiopia.
Kampuni hiyo inasema imeanzisha kituo cha kupata taarifa kuhusu familia na marafiki za watu waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
ege la Ethiopia- Ethiopian Airlines inasema walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adi Ababa.
Orodha ya abiria waliokuwa kwenye ndege ya #EthiopiaAirlines imetolewa
32 Kenya
18 Canada
9 Ethiopia
8 Chinese
8 Italian
8 American
7 France
7 British
6 Egypt
5 Netherlands
4 UN passport
4 Indian
3 Russian
2 Moroccan
2 Israeli
1 Belgian
1 Igandan
1 Yemeni