Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika, amepeleka mbele uchaguzi wa urais uliotakiwa kufanyika tarehe 8,april na kusema kuwa hatagombea tena,
Nia ya kugombea kwake ilizuia maandamano ya nchi nzima kwa wiki kadhaa sasa.

Ameongoza Algeria kwa miaka 20 sasa, lakini hajaonekana muda mrefu katika maeneo ya wazi , kutokana na ugonjwa wa kiharusi alioupata mwaka 2013.
Tarehe mpya ya uchaguzi haijatajwa bado, mabadiliko katika baraza la mawaziri yatafanyika hivi karibuni, taarifa iliyotolewa kwa niaba ya Bouteflika imetoa maelezo hayo.
Hakukua na tamko kuwa rais huyo atajiuzulu kabla ya tarehe mpya ya uchaguzi.
Rais BouteflikaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionwaandamanaji wakitumia picha za kukejeli kwa Rais Bouteflika
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Algeria Ahmed Ouyahia alijiuzulu na nasafi yake kuchukuliwa na waziri wa mambo ya ndani Noureddine Bedoui ambaye anakumbwa na kazi kubwa ya kutengeneza serikali mpya.
Bouteflika alisema nini?
''hakutakua na muhula wa tano'' ilisema taarifa kutoka kwa Rais Bouteflika, ''hakuna maswali katika hilo, ukizingatia hali yangu ya kiafya, na umri wangu, kazi yangu ya mwisho kwa watu wa Algeria ni kuhakikisha wanapata uongozi mpya'' aliendelea kusema katika taarifa yake.
Alisema wiki iliyopita kuwa kama atachaguliwa tena hatokaa sana madarakani atajiuzulu, lakini tamko hilo halikuacha watu kuandamana.
maandamanoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaandamano yalihamasishwa kupitia mitandao ya kijamii
Tamko la kutogombea kwa rais Bouteflika, limepongezwa na mataifa mengine, ikiwemo Ufaransa, ambapo waziri wa mambo ya nje, Jean-Yves Le Drian amesema ufaransa imefurahishwa na uamuzi huo na kuwa ni wakati wa kupata serikali mpya.
Kiongozi wa kwenye TV
Kwa mara ya mwisho alionekana akihutubia Umma mwaka 2014 -hotuba ya shukrani kwa raia wa Algeria kwa kuuamini utawala wake baaa ya kushinda uchaguzi uliokuwa umetangulia.
Aliahidi kutekeleza suala la mgawanyo wa madaraka, kuupa nguvu upinzani na kuhakikisha haki za raia zinafuatwa.
Baadhi waliona kuwa hii ni ishara ya mabadiliko ya sera katika uongozi , lakini hakua ushahidi wa kuonekana kwake kwa muda mrefu.
Raia wa nchi hiyo wamekua wakibahatika kumuona mara chache kwenye Televisheni akisalimiana na ujumbe kutoka nchi za kigeni wanaofika nchini Algeria.
Au kumuona kwenye ufunguzi wa mkutano mwaka 2016-akionekana amekaa kwenye kiti cha magurudumu, akionekana dhaifu, mwenye uchovu lakini mwenye tahadhari
Mpaka mwaka 2018,ikawa wazi kuwa Chama chake kimempendekeza kuwania tena uchaguzi wa mwaka huu.
Alikua kwenye ufunguzi wa Msikiti na vituo vya treni za umeme katika mji mkuu wa Algiers.Wiki chache baadae alikua kwenye ziara kutazama ujenzi wa Msikiti mkubwa wa tatu duniani uliogharimu dola za Marekani bilioni mbili.