Mtu mmoja nchini Marekani anadai kuwa amepata kanda ya video inayomuonesha mwanamuziki wa R. Kelly "akiwanyanyasa kingono wasichana wadogo wenye asili ya wamarekani weusi ."
Gary Dennis amewaambia wanahabari kuwa ameiwasilisha kanda hiyo kwa mamlaka za Marekani baada ya kuipata ndani ya nyumba yake.

R. Kelly alishitakiwa mwezi uliyopita na makosa kumi ya unyanyasaji wa kingono unaohusisha waathiriwa wanne watatu kati yao wasichana wadogo.
Msanii huyo wa muziki wa R&B amekanusha kuwa ndani ya video hiyo pamoja na tuhumu zote zinazomkabili
Akipatikana na hatia Kelly anakabiliwa na kifungo cha miaka saba kwa kila kosa..
Bwana Dennis,ambaye ni mhudumu wa makaazi ya watoto, amesema kuwa alipata kanda hiyo alipokuwa akipanga sanduku la video za zamani.
Aliamua kutazama moja ya video hiyo baada ya kuona imeandikwa jina "R. Kelly".
R Kelly performingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionR Kelly
Alitarajia kuona onyesho lake la zamani lakini badala yake alishangaa kuona picha za kingono anazodai zinamhuisisha msanii huyo.
Bila kuelezea kwa undani yaliyomo kwenye kanda hiyo, bwana Dennis anasema kuwa alimuon "[R. Kelly] akiwaambia wasichana hao kufanya alivyowaagiza kufanya na kuashiria kuwa ni yeye mwenyewe aliyekuwa akinasa video hiyo."
Anasema baada ya kugundua hilo alionelea ni ''wajibu wake'' wa kimaadili kuwafahamisha maafisa wa usalama.
Lakini kabla ya kufanya hivyo anasema kuwa aliwasiliana na wakili Gloria Allred,ambaye anawaakilisha wanawake wanaodai kudhulumiwa kingono na mwanamuziki R. Kelly.
Baada ya hapo kanda hiyo iliwasilishwa kwa waendesha mashtaka wa jiji la New York.
R. Kelly katika mahojiano na mtangazaji wa CBSHaki miliki ya pichaCBS
Bi Allred, amesema kuwa Dennis hakuwa na uhusiano wa kibinafsi na R. Kelly na kuongeza kuwa alipewa kanda hiyo na rafiki yake akifikiria maudhui yake ni ya matukio ya kitambo ya michezo.
Mapema mwezi huu nyota huyo wa miondoko ya R&B alinesha masikitiko makubwa kuhusiana na tuhuma dhidi yake katika kipindi kimoja cha asubuhi cha televisheni.
Kelly alikiri kufanya mambo mengi mabaya miaka ya nyuma lakini aliomba radhi kwa wanawake ambao alikuwa na mahusiano nao.
Kelly anaamini kuwa , ni rahisi sana kwa msanii kushutumiwa na madai mbalimbali, kitu ambacho watu wanafanya ni kupiga simu tu.