Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi  akipokea taarifa kutoka kwa katibu mkuu wa FEMA club mkoa wa Iringa mwalimu Fares Tunus wakati wa mahafali ya klub za FEMA yaliyofanyika shule ya sekondari ya wasichana ya Ifunda mkoani Iringa.
 Baadhi ya wanafunzi waliojitokeza kwenye mahafali hayo ya klabu za FEMA 
Mwenyekiti wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi  akiwa  katibu mkuu wa FEMA club mkoa wa Iringa mwalimu Fares Tunus  pamoja na wageni wengine wakelekea ukumbini kwenye sherehe za mahafali ya klabu za FEMA mkoani Iringa. 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mwenyekiti wa jukwa la walimu
wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi amewataka wanafunzi wa kike kujikinga na
mimba za utotoni ili kujijenga malengo mazuri ya hapo baada yenye tija kwa
taifa na wao binafsi.

Akizungumza wakati wa mahafali
ya club za FEMA yaliyofanyika katika shule ya sekondari ya Ifunda Girls,Ngowi
alisema wanafunzi wengi wa kike huacha masomo mapema kutokana na kupata mimba
wakiwa bado wapo masomoni hivyo ni lazima mjijengee malengo.

“nimetembea sehemu nyingi
nimekuta nimekutana na watoto wakike wengi wameacha shule kwa sababu ya kupata
mimba wakiwa shuleni,hivyo hata nyie mnatakiwa kujitunza na kuwa na maisha
mazuri na bora kama ambavyo mnatuana baadhi ya wanawake tunafanya vizuri kwa
kuwa  tulijitunza toka tukiwa shuleni” alisema

Ngowi aliwaambia,starehe na
mapenzi vipo siku zote za maisha hivyo lazima mjitambue katika umri huu ndio
muda wa kutengeneza dira ya maisha yenu hapo baadae kwa faida yenu.

“Kila mwanamke ambaye mnamuna
hivi sasa amefanikiwa ni kutokana na kujitunza walipokuwa wanasoma kama ambavyo
nyie mpo hivi sasa,mnatakiwa kujifunza kutoka kwa wanawake walifanikiwa”  alisema

 Aidha Ngowi aliwataka wanafunzi kuwa wazalendo
na maendeleo ya nchi yao kuwa kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa wamekuwa
kuwapotosha juu ya ukweli ambao unaendelea kwenye nchi hii,hivyo lazima muwe
wazalendo wa kweli kwa kuipenda nchi yetu na kuilinda isiingie kwenye
machafuko.

“Ili uweze kufanikiwa katika maisha
uzalendo ni japo la kwanza na la msingi kabisa kwenu nyie wanafunzi kwa kuwa ndio
taifa la sasa na baadae kwa kuwa mtakuja kuwa viongozi wa kuongaza nchi hii na
siwa watu wengi hata sisi ni viongozi ambao tulisoma katika shule kama hizi
ambazo nyie mnasoma hivi sasa” alisema

Akiwa katika mahafali hayo mwenyekiti
wa jukwa la walimu wazalendo Mkoani Iringa Merysina Ngowi aliwachangia viongozi
shilingi laki mbili kwa ajili ya kuwawezesha kuweza kufika katika maeneno
ambayo wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wanafunzi hao zaidi ya mia nane wa
mkoani Iringa.

Awali akisoma taarifa kwa mgeni
rasmi, katibu mkuu wa FEMA club mkoa wa Iringa mwalimu Fares Tunus alisema kuwa
wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha za kuendeshea semina
mbalimbali wa walimu walezi wa mkaoni Iringa.

“Tunakosa pia fedha za kuendeshea
matamasha mbalimbali yenye kubeba ujumbe mzuri katika jamii,ukosefu wa ofisi ya
FEMA mkoa wa Iringa” alisema

Tunus alisema kuwa mikakati yao
ni kuhakikisha wanaandaa mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi wananchama wa FEMA
yatakayo kuwa yanahusisha shule za sekondari tano za mkoa wa Iringa.

“Tutaendelea kushirikiana na
serikali katika kuwalea vijana katika maadili mema na kuhakikisha FEMA klabu
zinaenea katika shule zote za sekondari hapa mkopani iringa” alima Tunus