Serikali imetangaza tena ajira 736 za kada ya afya zilizokosa waombaji  wenye sifa huku wengi wakiwa ni wauguzi ngazi ya cheti.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,  Innocent Bashungwa ametoa taarifa hiyo leo Jumapili  Juni 26,2022 wakati akitangaza

waliochaguliwa katika ajira mpya zilizotangazwa na serikali mapema Aprili, 2022 mbapo walimu 9800 wamepatikana.

Kwa upande wa kada ya afya walitakiwa 7612 lakini waliopatikana ambao wana sifa ni 6876 na hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 736.

Bashungwa amesema kwenye kada hiyo wengi waliokosa sifa ni daktari wa meno 50, tabibu meno, tabibu wasaidizi, watekilonijia mionzi na wauguzi ngazi ya cheti.

“Nakuagiza katibu mkuu kuanza sasa katangaze nafasi hizo ili zianze kugombania na watu wenye sifa ili tujaze mapema kadri inavyowezekana ili wakawatumikie Watanzania,” amesema Bashungwa.

Kuhusu walioteuliwa kuanza ajira, amewataka kuripoti haraka kwenye halmashauri walizopangiwa kwani ndani ya siku 14 zoezi litafungwa na ambao warakuwa hawajaripoti ajira ao zitachukuliwa na wengine.


Kwa upande mwingine amesema waajiriwa hao wapya waripoti kwa waajiri wao na kupeleka taarifa zote muhimu ikiwemo vyeti vya taaluma ambavyo vitapelekwa kwanza Baraza la Mitihani kwa uthibitisho ili kubaini ambao watakuwa wameingia kwa kughushi.