Ukhty wetu Kipenzi Bi Twaiba Khaula pichani{katikati} akiwa na wageni wake maalumu katika picha ya pamoja hapo jana tarehe 25/06/2022 katika Dua aliyoiandaa kuwaombea wazazi,Wagonjwa,watu waliotangulia mbele za haki na wenye haja mbalimbali zilizofanyika katika kitongoji cha Ijmuiden nchini Uholanzi.
Ukhty wetu kipenzi cha watu Bi. Twaiba Khaula Ahmed akiwa anaingia ukumbini hapo jana siku ya jumamosi ya tarehe 25/06/2022 katika ukumbi wa Star Palace uliopo kitongoji cha Ijmuiden nchini Uholanzi.Ukhty wetu alifanya dua maalumu hapo jana katika kuwaombea dua watu mbalimbali wakiwemo wazazi,wagonjwa,marehemu waliotangalia mbele za haki na watu wenye shida zao mbalimbali.Pamoja na hayo Bi Twaiba Khaula  alifurahia sherehe yake ya kutimiza miaka 50 toka kuzaliwa kwake.
Mashekh wakubwa kutoka nchini Uingereza walishiriki katika kusoma dua maalumu za kuwaombea watu mbalimbali wakiwemo wazazi,wagonjwa mbalimbali,ndugu na jamaa waliotangulia mbele za haki.
Shekh Fuad Al-Badoza kutoka nchini Uingereza alishiriki katika kisomo maalumu cha kuwaombea wazazi wetu walio hai,waliotangulia mbele za haki,wagonjwa mbalimbali na watu wenye mambo mazito Mungu awafanyie yawe mepesi na kuwasihi waislamu kusameheana bila kuwekeana vinyongo ili Mungu awe radhi na umma wake.shughuli nzima ya kuomba dua hiyo ilifanyika siku ya jumamosi ya tarehe 25/06/2022 katika kitongoji cha Ijmuiden nchini Uholanzi .