Rajabu Abdul Kahali almaarufu Harmonize akiwa na mpenzi wake Kajala.

 

Rajabu Abdul Kahali almaarufu Harmonize; ni supastaa wa muziki nchini Tanzania ambaye anafanya vizuri zaidi kwa sasa kiasi cha kuwapa homa washindani wake wa upande wa pili, Gazeti la IJUMAA lina exclusive.

 

Siku chache baada ya kumchumbia staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja au Fridah Kajala, Harmonize au Harmo anasema kuwa, mpaka sasa bado haamini kama anamiliki mwanamke anayependa kwenye chini ya jua hili.

 

Harmonize au Konde Boy anasema kuwa, ndiyo maana haachi kumshukuru Mungu kwa alichokifanya kwake.

HARMONIZE FURAHA KAMA YOTE

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Harmonize anasema kuwa, hakuna kitu kizuri kama kuwa na mwanamke ambaye unampenda kutoka ndani ya moyo wako ambaye akiishi na wewe unapata furaha ya ukweli na mambo yako yanakwenda vizuri.

 

Konde Boy anasema kuwa, kwa upande wake amepata furaha ya kudumu ya maisha yake baada tu ya Kajala kukubali kuwa wake kwa mara ya pili baada ya kuwa pamoja mwaka jana na kuachana kisha kurudiana hivi karibuni.

 

HARMONIZE HAAMINI

“Kuna wakati mtu huamini kabisa kinachotokea kwenye maisha yako, mimi siamini kabisa kama K (Kajala) ni wangu sasa.

“Mwenyezi Mungu ni mwema sana, amenisogeza karibu kabisa na mwanamke wa maisha yangu, maana nitampenda siku zote, nampenda mno furaha ya maisha yangu ipo mikononi mwake sasa,” anasema Harmonize ambaye wiki iliyopita alimvalisha pete ya uchumba Kajala na harusi ipo mbioni.

 

KAJALA NA HARMO WANAFUATILIWA ZAIDI

Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umebaini kwamba, kapo ya Kajala na Harmonize kwa sasa ndiyo kapo inayofuatiliwa zaidi na kupendwa na wengi ukilinganisha na kapo nyingine za mastaa Bongo.

Kwa mujibu wa Harmonize, hakuzoea matunzo na mambo mazuri na mazito ambayo anayapata sasa hivi kutoka kwa Kajala.

 

Kwa mfano; kabla ya kurudiana na Kajala, Harmonize hakuonekana akishukuru kwa kupatiwa matunzo, lakini sasa anatupia tu vipande vya video akifurahia usafi na misosi mizuri kutoka kwa mwanamama huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Paula Paul au Pau.

 

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Kajala na Harmonize akiwemo Mwijaku, jamaa huyo hakuzoea staili hiyo ya maisha na zaidi sana alikuwa akiishi kigetogeto, lakini sasa anapendeza na kunawiri.

 

“Harmonize hakuwa hivi alivyo, mambo ya vyakula vya mtaani Kajala amesema hakuna, sasa Harmonize anapendeza, hanywi tena pombe, anakunywa soda na maji tu,” anasema Mwijaku.

Katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA, Harmonize au Jeshi ambaye ni Mkurugenzi wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide anasema kuwa, ameingia mzimamzima kwa Kajala na anaamini ndiye alikuwa chaguo lake sahihi.

 

Hata hivyo, Harmonize anamtahadharisha Kajala kwamba kama ataleta mambo yasiyoelewa kwenye mapenzi yao hayo, basi ajue anatembea na damu ya moyo wake hivyo kuendelea kuishi itakuwa ni ngumu.

Stori; Imelda Mtema, Dar