Wakati mzozo mkali juu ya mapigano ukiendelea baina ya Korea ya Kaskazini na Korea Kusini nchi ya China imetoa mapendekezo yake kama ushauri kufanyike mazungumzo ya dharura, baina ya mataifa sita yaliyohusika na upatanishi katika mpango wa nuklia wa Korea Kaskazini.
Afisa mmoja wa China, aliwaambia waandishi wa habari mjini Beijing, kwamba China ina wasiwasi mkubwa kuhusu yaliyotokea hivi karibuni katika Rasi ya Korea na inataka mataifa sita, Marekani, Urusi, Japani, China yenyewe na Korea mbili, yakutane mwanzo wa mwezi ujao.Lakini Korea Kusini imesema huu si wakati wa kurejea tena kwenye mazungumzo ya pande hizo sita.
0 Comments