Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jan 20, 2018

BALOZI JOSEPH SOKOINE KUKUTANA NA WATANZANIA WIKI IJAYO 27.01.2018

0 Maoni
Mh:Balozi Joseph Edward Sokoine

TANGAZO
Kwa watanzania wote wanaoishi nchini Ubelgiji na vitongoji vyake wanaarifiwa kuwa tarehe 27.01.2018 siku ya jumamosi saa nane kamili mchana katika mji wa Antwerpen Mh:Balozi Sokoine atakutana na watanzania wote ili kusikiliza kero,matatizo,ushauri na mengineyo.Kila mmoja ni fursa yake kufika kwenye mkutano huu ili kusikiliza na kutoa mchango wake wa mawazo aliyonayo.Mahala pa mkutano ni ukumbi wa Gemeente  Luchtbal Antwerpen.
Kufika kwako kutasaidia sana mchango wa Taifa.Yeyote atakayeliona tangazo hili tafadhali tusaidie ku'share na wengine walione ili waweze kufika katika mkutano huu.

Read More >>

Waziri Mkuu azuia mali za chama cha ushirika KNCU kuuzwa

0 Maoni
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira asitishe uuzwaji wa mali za Chama cha Ushirika cha Kilimanjaro (KNCU).
Read More >>

Serikali yazifutia usajili meli 2 zilizonaswa na dawa za kulevya

0 Maoni
SERIKALI imezifutia usajili meli mbili zilizokamatwa kwa kupakia shehena za dawa za kulevya na silaha kinyume cha sharia, huku zikiwa zinapeperusha bendera ya Tanzania. Aidha imesema itaanzisha utaratibu wa kuzifanyia uchunguzi wa kina meli zote mpya zitakazoomba usajili pamoja na wamiliki wake kwa kushirikisha vyombombalimbali vya serikali, vikiwemo vile vya ulinzi na usalama ili kuondokana na utata na dosari zinazoharibu sifa njema ya nchi.
Read More >>

Mganga awapa mimba hewa wanawake 700

0 Maoni
POLISI nchini Guinea imesema inamshikilia mganga wa kienyeji anayetuhumiwa kuwalaghai mamia ya wanawake, kuwa watapata mimba. Mganga huyo, N’na Fanta Camara aliwapatia wanawake hao ambao hawakuwa na uwezo wa kupata ujauzito majani mchanganyiko na mimea mbalimbali, iliyosababisha matumbo ya wanawake hao kufutuka na kuonekana kama wana mimba.
Read More >>

Wanawake wadaiwa kubakwa baada ya kujifungua hospitalini Kenya

0 Maoni
Waziri wa afya nchini Kenya Dkt Cleopha Mailu ameamrisha uchunguzi kufanywa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta baada ya wanawake waliojifungua kudai kwamba wanadhalilishwa kingono.
Read More >>

Mnangagwa: Mugabe alisahau alikuwa amenifuta kazi

0 Maoni
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema mtangulizi wake Robert Mugabe alikuwa amesahau kwamba alikuwa amemfuta kazi kama makamu wake.
Amesema waliwasiliana wakati wa mzozo ambao hatimaye ulipelekea kuondolewa kwake madarakani.
Read More >>

NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO KUTAMBUA UMUHIMU WA KULIPA KODI

0 Maoni
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza jambo wakati wa mkutano na wachimbaji wa madini ya Jasi na Chumvi Mkoani Mtwara, Leo 19 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Read More >>

Mkutano Mkuu Wakuifufua Upya Jumuiya ya Watanzania Washington DC

0 Maoni
Watanzania waishio Washington DC na Vitongoji vyake, siku ya Jumapili Jan 14, waliweza kufanya maamuzi ya kuifufua tena Jumuiya ya Watanzania DMV, ilivunjika kwa zaidi ya miaka miwili hadi kufikia kufanya maamuzi ya kuifufua tena upya Jumuiya hiyo.
Read More >>

UZINDUZI WA MBIO ZA 21KM TIGO KILIMANJARO MARATHONI MOSHI MJINI JANA

0 Maoni
​Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo kanda ya Kaskazini ,Henry Kinabo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Msimu wa 16 wa Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018,Uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace Homes mjini Moshi,Mashindano ambayo Kampuni ya Tigo inadhamini Mbio za Nusu Marathon ,Km 21.
Read More >>

Jan 19, 2018

Upashaji tohara wa wanawake: Daktari ataka ukeketaji uhalalishwe Kenya

0 Maoni
Daktari mmoja nchini Kenya amewasilisha kesi mahakamani akitaka upashaji tohara wa wanawake ambao hufahamika pia kama ukeketaji uhalalishwe.
Dkt Tatu Kamau anasema sheria inayoharamisha ukeketaji wa wanawake na wasichana inakiuka utamaduni katika jamii nyingi za Kiafrika.
Read More >>

Uingereza yamteua waziri wa upweke

0 Maoni
Uingereza imemchagua waziri wa upweke ili kukabiliana na kile ambacho waziri mkuu wa Uingereza{pichani juu} amedai ni uhalisia wa masikitiko kuhusu maisha ya sasa yanayoathiri mamilioni ya watu.
Read More >>

Waziri mkuu wa New Zealand mwenye umri wa miaka 37 asema ni mjamzito

0 Maoni
Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amefichua kwamba yeye ni mjamzito.
Bi Ardern alisema kwamba yeye na mpenzi wake Clarker Gayford walikuwa wakitarajia mwana wao mwezi Juni ambapo baadaye atachukua likizo ya wiki sita.
Read More >>

Tanzania yafuta usajili wa meli mbili za kigeni zilizokuwa na mihadarati

0 Maoni
Serikali ya Tanzania imetangaza kuunda kamati ya pamoja ya wataalam bara na visiwani itakayoshirikisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kupitiwa upya usajili uliokwishafanyika na kuzihakiki taarifa za meli zote zilizosajiliwa nchini, kuangalia mwenendo mzima wa usajili, na hatimaye kutoa mapendekezo na ushauri kwa Serikali.
Read More >>

Jan 18, 2018

MHE BITEKO AMUAGIZA KAMISHNA WA MADINI KANDA YA KUSINI KUANZISHA OFISI YA MADINI WILAYANI RUANGWA

0 Maoni
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Read More >>

Korea kusini yasema iko macho kwa kaskazini

0 Maoni
Korea kusini imesema itashughulika na Korea kaskazini kwa kile alichokiita '' Macho ya wazi'' baada ya kukamilika mpango wa kuweka timu moja ya pamoja katika michezo ya majira ya baridi ya Olympics inayofanyika mwezi ujao.
Read More >>

Polisi Tanzania yakana taarifa upigaji marufuku vimini

0 Maoni
Polisi nchini Tanzania, imekanusha taarifa zilizoenea kwamba imepiga marufuku uvaaji wa nguo fupi au 'miniskirt' na vile vile nguo zinazobana. Kamanda wa polisi Mkoa wa Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema taarifa hizo ambazo zimeandikwa katika moja ya magazeti nchini sio za kweli, na "zimetengenezwa" na "kuchongwa" kwa lengo la kutafuta umaarufu.
Read More >>

Kunguru alazimu ndege ya wanajeshi wa AMISOM kutua Burundi

0 Maoni
Kunguru mmoja amelazimu ndege iliokuwa imewabeba wanajeshi wa Amisom kutoka Burundi kutua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa Bujumbura nchini Burundi.
Read More >>

Jan 17, 2018

NAIBU WAZIRI WA MADINI MHE BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI WADOGO WA GYPSUM KUWA NA UMOJA

0 Maoni
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akiwasili kijiji cha Hoteli Tatu, Kata ya Mandawa Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi kwa ajili ya kuembelea kampuni ya Universal Mining Ltd kujionea hali ya uzalishaji wa jasi (Gypsum) unavyoendelea wakati wa ziara ya Siku tatu katika Mkoa wa Lindi na Mtwara, Leo 17 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Read More >>

MWENYEKITI WA UVCCM KHERI D JAMES AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI MBALI MBALI WA UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM

0 Maoni
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri Denis James(MCC) akizungumza  kwa Msisistizo wakati wa kikao na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya mkoa wa dar esa salaam pamoja na Baraza kuu la Vijana Wilaya ya Kinondoni, kulia ni Kaimu Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Mussa Kilakala,Katika Ofisi ndogo ya Makao makuu ya UVCCM Upanga Dar es Salaam.
Read More >>

WCF YAWANOA WAAMUZI, WASULUHISHI NA MAKATIBU MUHTASI KUTOKA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI (CMA)

0 Maoni
 Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, (kushboto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba,
Read More >>
 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP