Dunia inaanza kuwaka moto kwa staili tofautitofauti sasa.
Gambia imesema inakatisha uhusiano wake na Iran, na kuwataka wawakilishi wote wa serikali ya Iran waliopo Gambia kuondoka katika kipindi cha saa 48.
Maafisa wa taifa hilo dogo la Afrika Magharibi, hawajatoa sababu ya kuchukua hatua hiyo.
Hata hivyo, mwezi uliopita Nigeria ilisema imekamata shehena ya silaha zinazosafirishwa kinyume cha sheria, ambazo inadaiwa zilikuwa zikipelekwa nchini Gambia.

Shinikizo

Afisa wa ngazi ya juu wa Iran Alaeddin Borujerdi amesema hatua hiyo ya Gambia imechukuliwa kutokana na shinikizo kutoka Marekani.
Mamlaka za Nigeria zilisema zilikamata silaha hizo zikiwemo mabomu ya kurushwa na roketi na mabomu ya kurushwa kwa mkono,zikiwa katika makontena yaliyoandikwa kuwa yana vifaa vya ujenzi.