Mchakato wa utekelezwaji wa katiba mpya nchini Kenya, umepata pigo kubwa baada ya wabunge kukataa kuidhinisha makamishna wa tume mbili muhimu waliokuwa wamependekezwa.
Wabunge walisema orodha hiyo haijazingatia uwakilishi wa mikoa yote na inapaswa kurejeshwa kwa Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga.Wabunge pia walikataa kuidhinisha kamati iliyopendekezwa kusimamia ugawaji wa rasilimali.
Kufuatia uamuzi huo wa wabunge, huenda ikatoa fursa kwa kwa raia yeyote wa Kenya kwenda mahakamani kuwasilisha kesi ya kutaka bunge livunjwe.
Hata hivyo wataalamu wa masuala ya sheria nchini Kenya,wanasema uamuzi huo wa wabunge huenda ukasababisha mzozo wa kisiasa na kikatiba.
0 Comments