Watoto walikuwa na furaha muda wote,walipiga zile kwetu tunazokatwaza kupiga'Fataki'ilikuwa muda wa mchana siku moja kabla ya mwaka mpya,yani mitaani kwa kweli kulikuwa kuzuri kwa kuwa kila mmoja alikuwa ni mtu wafuraha.
Hili sio duka la baiskeli jamani,wala sio kwa fundi baiskeli,hapa ni parking ya baiskeli ambayo haina malipo wala kuibiwa,baiskeli,unaweka baiskeli yako kisha unajiondokea tu.Kwa kweli waungwana wa mkoa huu ni watu waazuri sana.
Ukiangalia chini ya Lami huwezi kuona hata karatasi,Hapa ni kituo cha mabasi ambapo kuna kila usafiri,kwani mabasi yanafanya usafiri sehemu tofautitofauti,madereva wake ni wakarimu na wasikivu pale unapowauliza.
Mitaani kumepambwa na kupambika kiukweli,kwa kweli wenzetu wanajua nini maana ya mwaka mpya.Maduka ufunguliwa mpaka usiku wa saa tatu kwani ni kipindi kizuri sana kufanya shopping usiku.Nilizunguushwa sana na wenyeji wangu.Watu njiani walikuwa na ukarimu kwa kila mmoja.