Umeme na maji hali haitakuwa shwari hapa nchini - mikoa itakayoathiriwa na hali hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Mwanza, Mara, Mbeya, Iringa, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga na Tanga.
Alisema mafundi wanaendelea na matengenezo ya mashine hizo kuhakikisha hali ya inarudi kuwa ya kawaida ili kumaliza tatizo la mgao wa umeme.
Katika kukabiliana na tatizo la mgao katika mikoa hiyo Tanesco imewasha mashine mbili za IPTL za jijini Dar es Salaam ambapo megawati 50 zitazalishwa.
Alisema wamelazimika kuwasha mashine mbili za IPTL kutokana na gharama kubwa za mafuta ambazo zingeweza kutumika kama wangewasha zote.
Baada ya mashine za IPTL zitasaidia kupunguza tatizo na hivyo kuacha pengo la Megawati 100 kati ya 150 zilizojitokeza kutokana na kuharibika mitambo ya kuzalisha umeme.
Hali ya umeme ikiwa tete kiasi hicho na kulazimisha matumizi makubwa ya jenereta katika uzalishaji na utoaji huduma katika mikoa hiyo, athari za kiuchumi zinabashiriwa kunyemelea taifa kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.
Hali hii inatokea wakati kukiwa na hofu ya kutokea kwa upungufu mkubwa wa maji katika mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme kutokana na kutokunyesha kwa mvua za vuli mwaka huu, ingawa bado bwawa kuu la Mtera linalipotiwa kuwa na maji yakiwa na kina cha mita 693.11 chini ya kiwango cha juu cha mita 698.3.
0 Comments