Ukiangalia vizuri utaona kwamba magari kwa upande huu na upande ule yamesimama yakisubiri waendao kwa miguu wavuke kisha nao ndipo waendelee na safari zao.Angalia vizuri unaweza kuona mabibi walio nyuma wanapiga soga kabisaa na ma mama wa mbele nao stori zanoga kiasi kwamba mwingine kageuza hata shingo nyuma.Je kwetu kuna utaratibu kama huu kweli?Utabebeshwa matusi ya nguoni na madereva au hata makondakta wa daladala kwa njisi walivyokosa nidhamu.Kwa ulaya dereva yoyote ukimgonga mwenda kwa miguu kwenye kivuko unapigwa faini isiyopungua euro(yuro)15'000 cash na kunyan'ganywa leseni yako kwa muda usiopungua miaka 5 bila kuendesha gari,je hizi sheria nazo zingepelekwa kwetu Nahisi ajali zinazohepukika zingepungua sana tu.
0 Comments