Sakata la tuhuma za kulawitiwa kwa mtoto wa miaka 12 mkazi wa mjini hapa, sasa linaelekezwa kwa mwanasheria wa serikali wa kanda ya Songea, anayedaiwa kulififisha shauri hilo.
Awali shutuma zilielekezwa kwa jeshi la polisi mkoani Ruvuma, ambalo hata hivyo lilijiweka kando mwa shutuma za kumlinda mtuhumiwa wa kashfa hiyo.
Sajenti Yassini Kalumbi awa jeshi la magereza mbaye ni mzazi wa mtoto huyo (jina tunalihifadhi), aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa anasikitishwa na `kupigwa danadana’ kwa shauri hilo, kunakofanywa na ofisi ya mwanasheria huyo.
kwa habari zaidi...Kwa mujibu wa Kalumbi, ofisi ya mwanasheria huyo inaendelea kulishikilia jalada la kesi ya mwanaye anayedaiwa kulawitiwa Novemba 11, mwaka huu.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa wa shutuma hiyo yupo huru mitaani, na hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yake. Mtuhumiwa huyo ni mganga wa tiba asilia anayesadikiwa kuwa mmoja wa marafiki wa familia ya Kalumbi.
Inadaiwa kuwa siku ya tukio, mganga huyo alimuomba mtoto amsindikize nje ya nyumbani kwao, na kabla hawajafika mtaa wa pili walikuta kichaka ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kuchomoa kisu mfukoni na kuanza kumtishia, kisha kumlazimisha avue suruali na kumwingilia kinyume na maumbile.
Inaelezwa kuwa baada ya kumaliza kufanya unyama huyo, mtuhumiwa alichomoa uume wake na kumlazimisha mtoto huyo aunyonye, huku akiendelea kumtishia kisu na kumtolea lugha za vitisho.
Kalumbi anadai kuwa baada ya tukio hilo, mtoto huyo alirudi nyumbani peke yake, huku akiwa mnyonge na alipoulizwa, alieleza tukio lilivyokuwa, ndipo wakamchunguza sehemu za siri kwenye makalio na kukuta `ameumizwa’.
Kwa upande wao baadhi ya wanachi mjini hapa wameelezea kusikitishwa kwao kutokana na hali iliyojitokeza kuhusiana na tukio la kulawitiwa mtoto huyo.
Taarifa ya ofisi ya mwanasheria wa serikali kuhusu shutuma hizo, ilisema jalada la kesi hiyo limeshapokewa, lakini bado haijulikani ni lini kesi hiyo itapelekwa mahakamani kwa vile uchunguzi wa kishahidi kwa pande zote haujakamilika.
Mwanasheria wa Seriakali wa Kanda ya Songea, Edson Mwaruvanda, alisema hawawezi kukurupuka kuipeleka kesi hiyo mahakamani, kwani ushaidi wa Daktari hauna uzito mahakamani, na kesi hiyo inaweza ikatupwa ikiwa wahusika wakuu hawatapatikana.
0 Comments