Pichani steven Kanumba akiwa mjini Kigali nchini Rwanda,jinsi alivyolakiwa huwezi amini kwamba wasanii wa watanzania wanapendwa sana Rwanda.
Ni ukweli husiopingika kuwa tuna watu wanaoiwakilisha nchi yetu vyema kwa taaluma tofautitofauti,Ukiachilia wanamuziki wetu wa kizazi kipya ambao wapo juu sana katika kupeperusha jina la nchi yetu kwa njia ya mziki wao.sasahivi tuna nyota ambao wanakubalika Africa. kuna kundi la ze komedi orijino na kuna nyota wetu wa filamu ambao wanafanya kazi zao vizuri kiasi kukubalika nje ya nchi.
Kundi la ze komedi Orijino ambalo linatamba Afrika.Diamond mwenye kofia ya Bluu ni Mtanzania aliyefanya vyema sana mwaka huu katika uimbaji wake kiasi kwamba akachaguliwa akashiriki kugombea nafasi ya nyimbo bora za mwaka kwenye MTV MAMA africa jijini Lagos nchini Nigeria.
Kwa pamoja tuthamini kazi zetu na kuwajali wasanii wetu,kitendo cha kuwaponda na kutowajali wasanii wetu haipendezi kabisa.Ikiwa wanapewa heshima kubwa kila nchi wanazokwenda kwanini nasisi nchini tusiwaheshimu?Tuache kasumba ya kupondana na tuendelee kupeana moyo,turekebishane penye mapungufu na tuahakikishe bendera yetu inapepea Africa nzima na Duniani kwa ujumla.Nina imani na wewe ukikaza uzi utafanikiwa kwa fani uliyonayo.Maganga One.
0 Comments