Mazungumzo yanaendelea Arusha, makao makuu ya Jumuia ya Afrika mashariki nchini Tanzania, juu ya uwezekano wa kuwa na sarafu moja kwa eneo hilo la Afrika.
Maafisa wanaowakilisha Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, wanakutana kwa siku nne kujadili jinsi sarafu hiyo ya pamoja namna itakavyoafikiwa.Hii na awamu ya tatu ya kujaribu kuziunganisha nchi za Afrika kwa lengo la kurahisisha na kupunguza gharama za biashara.
Lakini wadadisi wamesema mradi huo utaleta wasiwasi katika eneo hilo kusipozingatiwa kuwepo kwa umoja wa kisisasa kwanza.
Kutoa kushoto ni Raisi wa Uganda bwana Yoweri Museven,Mwai Kibaki wa Kenya,Paul Kagame wa Rwanda,Jakaya Kikwete wa Tanzania na mwiso kulia ni Pierre Nkurunzinza raisi wa Burundi.Hawa ndio maraisi wanaounda umoja wa Africa Mashariki.MUNGU IBARIKI AFRICA NA WATU WAKE.
1 Comments