Pichani mshitakiwa Mohammed Ahmed Hussein ni mmoja wa watuhumiwa wanaoshtakiwa kuwafyatulia risasi waumini walipokuwa wakiondoka kwenye misa ya mkesha wa Krismasi, katika mji wa Naga Hamady kusini mwa Misri.
Watu wengine wawili wanaohusishwa na mauaji hayo watahukumiwa baadae.
Watu hao walikamatwa mara baada ya shambulio hilo, lakini kesi yao imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara.
Hukumu hiyo imetolewa wiki mbili tu baada ya shambulio la bomu la kujitoa mhanga nje ya kanisa la Copti katika mji wa Alexandria lililouwa watu 23.
Kesi hiyo imeleta chuki miongoni mwa jamii ya Wakristo wa Copti kwa sababu imechukua muda kumshitaki mtuhumiwa huyo ambaye anadhaniwa kuwa na uhusiano na mbunge wa chama tawala.
Hukumu hiyo ya kifo imetolewa wakati kuna wasiwasi mwingi kati ya jamii ya waislamu na wakristo nchini humo.
Mahakama ya usalama ya taifa huko Misri imetoa hukumu ya kifo kwa muumin wa kiislamu kwa kosa la kuua wakristo sita wa madhehebu ya Copti na polisi mmoja mwaka uliopita.
0 Comments