Maandamano yalianza kama mzaha japo Serikali ilipinga hii kitu.Wanachama na viongozi wa Chadema walipinga kauli hiyo.Walianza maandamano kama mnavyoona pichani.
Kikosi maalumu cha kuzuia ghasia kilisimamisha maandamano hayo,pichani wananchi wenye mabango wakiwa wamezuiliwa na askari wa FFU na askari wa usalama barabarani ila kama ujuavyo siku wananchi wanavyopatwa na jazba hali huwa si shwari.
Bado malumbano yakiendelea baina ya wana Usalama na Raia wenye hasira kali jijini Arusha.
Kikosi cha kutuliza ghasia kikiwa kimeshaanza kazi rasmi kama ujioneavyo mwanamama ambaye inasemekana ni mke wa kiongozi wa ngazi za juu Chadema(jina hatuna uhakika)akiwa anamwagika damu usoni kwa kile kinachosemekana ni kipigo toka kwa wana usalama hao.
Akionyesha hali ya kutokukubali na hali ile aliona bora afe kuliko kuonewa,aliendelea kuifuata gari ya wana usalama wale.Hatuji nini kiliendelea mbeleni,tutawaletea maelezo kadri tunavyoyapata.
Wana usalama kikosi maalumu cha kuzuia ghasia FFU kikiwa kimezingira kila kosa kuhakikisha kuwa hakuna maandamano wala ghasia zikiendelea jijini Arusha.
Sio kama analia kwa kupigwa,ila ni hali ya mabomu ya machozi iliyotawala maeneo fulani jijini hapo na kuwafanya baadhi ya wananchi kulia bila kupenda.
Doria ya wana Usalama ikiwa inazungukia jiji la Arusha kuweka hali ya usalama kwa raia wasio na hatia sawa.Blog inawatakia watu woote walioumia katika tukio hili wapone haraka na waliokamatwa pia waachiwe na wawe huru na kuendelea na shughuli zao kama kawaida,Blog inaiombea nchi hali ya utalivu na kuwataka viongozi wa Chadema kuwa wasikivu na kukubaliana na matokeo yaliyotolewa na Serikali kwani bila kufanya hivyo hali ya hatari itakuwapo nchini kitu ambacho hatukitaraji kitokee.Wananchi tuwe wasikivu na kukubali matokeo.
0 Comments