Jamaa mmoja anapiga simu ofisi ya makumbusho ya Taifa.
"Haloo hapo ni makumbusho ya taifa?
OFISI:Ndio tukusaidie nini?
JAMAA:"Ok, naomba mnikumbushe mwaka juzi saa yangu niliipoteza wapi?"
OFISI:"Pumbavu hiyo siyo kazi yetu"
JAMAA:Sasa makumbusho mnakumbusha nini?"
OFISI:Tunahifadhi mambo ya zamani.
JAMAA:"Ahaa.....kumbe saa yangu mtakuwa nayo!" Nakuja kuichukua sasa hivi.