Mshindi wa pili wa shindano la Bongo Star Search 2008, Rogers Lucas yuko mbioni kuanzisha darasa la muziki kwa lengo la kuinua sanaa hiyo.
Akizungumza Rogers ambaye katika BSS 2008 alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake wa kuimba na kupiga gita, alisema kuwa amefikia uamuzi wa kufundisha muziki kwavile anaamini kuwa anaweza kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji kujifunza mbinu za kuandaa kazi zao kitaalam.
Alisema darasa hilo litakuwa katika eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam na atashirikiana na msanii mwenzake aitwaye Wazee.
Hivi karibuni, Rogers aliyejifunza muziki katika nchi za Swaziland, Ujerumani na Austria, ametambulisha wimbo uitwao ‘Tulizana’, alioshirikiana na Maunda Zoro na kuandaliwa Allan Mapigo.