TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars juzi ilibanwa mbavu na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Burundi katika michuano ya Bonde la Mto Nile.

Burundi ilifunga bao la kuongoza katika dakika ya 49 kupitia kwa Tambwe Hamisi aliyefunga kwa kichwa cha chinichini baada ya kuunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Didier Kavumbabo.