Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeanza vibaya mashindano ya kumtafuta bingwa wa Bonde la Mto Nile baada ya kula Mkon'goto wa bao 5 - 1 dhidi ya wenyeji timu ya taifa ya Misri.Mashindano hayo yanashirikisha nchi saba za Afrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa Chama cha Soka cha Misri (EFA), Samir Zahir alisema bingwa atapata pauni milioni moja ya Misri (ambayo ni zaidi ya Sh. Milioni 250) za Tanzania wakati mshindi wa pili atapata pauni 700,000 za Misri (zaidi ya Sh.Milioni 176), na wa tatu pauni 600,000 (zaidi ya Sh. Milioni 150).
"Tumetoa zawadi hiyo kuhamasisha zaidi timu, kucheza kwa nguvu ili kuboresha mashindano yetu ambayo ni mara ya kwanza kufanyika," alisema rais huyo.
Aliongeza kuwa kutakuwa na zawadi za mfungaji bora, kipa bora na mchezaji bora... ni aina ya mashindano ambayo tunataka yawe mfano Afrika," alisema Samir.
HAYA TUMEANZA VIBAYA MASHINDANO,BINAFSI NASEMA MWANZO SIKU ZOTE NI ....