Akipata picha ya pamoja na wake zake wote wapatao 39 Bwana Ziona Chana anajisifia kwa kuona fahari kwakuwa na familia yenye upendo.
Bwana Ziona mwenye wake 39, watoto 94 na wajukuu 33 Kwa ujumla wote kwa pamoja akijiwajulisha unapata watu 181 ambao hata kwenye kuchukua picha ilibidi wengine wasuburi kidogo kwani ilishindikana kuwapata wote kwa pamoja.
 Huu ndio mjengo alioujenga  kijijini Batwang mjini Mizoram nchini India wenye vyumba 100 ili kukidhi mahitaji ya kulala familia yake yote.ameupa jina la Ziona Minsion,ni jengo kubwa sana kwa kijijini hapo.Pichani chini baadhi ya wake zake wakiwa na kuku na mbogamboga pamoja na mchele kwenye hako katolori tayari kwenda kuandaa maakuli,Inasemekana wanatumia kuku 30 kwa mlo mmoja tu wa usiku.