Katika hali ya kusikitisha na kuona kwamba kuna watu wana roho za ajabu sana,Mwanamke mmoja analiyejulikana kwa jina la Faida Mwapili mwenye umri wa miaka 26 anashilikiwa na dola (Polisi) kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake wa kumzaa mwenyewe mwenye umri wa mwaka 1 ndani ya mto mpaka kufa.Akijieleza kwa masikitiko bidada huyo "Nimemtupa mtoto wangu kutokana na hali ngumu ya maisha inayonikabili hivi sasa,baba mtoto wangu kanikimbia hivyo nimeona ni bora nimtupe huyu mtoto nikizani nitapata wepesi kidogo wa maisha"alimalizia.Polisi bado wanamshikilia kwa uchunguzi zaidi kabla hawajamfikisha mahakamani.