Jana usiku kila mwananchi aliyekuwa na makazi karibu na kambi ya Jeshi GongolaMboto alikimbia alipopajua yeye,Wazazi waliacha watoto wao,walioweza kukimbia walikimbia,kuna waliokuwa wakianguka na kukanyagwa na wenzao kwa jinsi hali ilivyokuwa jijini hapo.Chanzo cha Milipuko ya mabomu hayo bado hakijatangazwa mpaka hivi sasa,ila kuna ajeruhi wengi walioumia.Athari na milipuko hiyo imetokea katika ghala namba 5 la Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) Gongolamboto.