HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala, imefuta utaratibu wa kutumia makandarasi katika uzoaji taka na badala yake, kazi hiyo itafanywa na halmashauri hiyo ili kutekeleza mkakati wa kuweka maeneo yake safi. Meya wa Manispaa hiyo, Jerry Silaa alisema, ili kutekeleza mkakati huo wa miezi mitatu, tayari manispaa hiyo imeshapokea magari maalumu sita kwa ajili ya uzoaji wa taka.