Waziri mkuu wa Misri, Ahmed Shafiq, ameomba msamaha kwa makabiliano yaliotokea usiku kucha katikati mwa mji wa Cairo.
Watu wawili walipigwa risasi wakati wa mapigano kwenye eneo la wazi la Tahrir kati ya wafuasi wa rais Hosni Mubarak na wapinzani wake.

Serikali imepinga madai kuwa ilikuwa imekusanya watu kutekeleza mashambulizi.
Viongozi wa mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uhispania wamesema wanafuatilia kwa karibu hali ya mambo nchini Misri.

Machafuko yaliozuka siku ya Jumatano yamezua maswali kuhusiana na uongozi wa Misri.
Mashambulizi yaliotekelezwa dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakishinikiza rais Hosni Mubarak kuondoka mamlakani yamezua tetesi kwamba huenda chama cha rais Mubarak kiliyapanga.
Afisa mmoja wa chama hicho ameshutumu wenzake kwa kupanga ghasia hizo. Kulingana na wizara ya afya, watu watano walifariki kwenye vurugu hizo huku wengine
Kwa upande wa jeshi, kuna hofu kwamba tayari limegawanyika.Wanajeshi hawakuchukua hatua yoyote wakati wafuasi wa rais Mubarak walipowashambuliwa waandamanaji.
Ingawaje awali jeshi lilikuwa limekiri kwamba kuna umuhimu wa kuwepo kwa mabadiliko ya kisiasa, msemaji wa jeshi siku ya Jumatano alitoa wito kwa waandamanaji kurejea nyumbani.
Hata hivyo kuna ripoti kwamba sasa jeshi linajaribu kutuliza hali.
Hofu iliopo kwa sasa ni kwamba migawanyiko serikalini huenda ikachelewesha hatua muhimu za kutuliza hali kuchukuliwa.