Rais Barrack Obama wa Marekani amekashifu machafuko yanayo endelea nchini Libya, katika hotuba yake ya kwanza kwenye runinga tangu mageuzi yaanze nchini Libya, yapata wiki moja sasa.Amesema kuwa ukatili unaotumiwa na vyombo vya serikali kukabili waandamanaji haukubaliki kamwe na kuwa serikali yake inatathhmini hatua za kuchukua.
Huku hayo yakiarifiwa maelfu ya waandamanaji wanaopinga serikali wamekuwa
wakisherehekea kile wanachokiita ushindi mkubwa Mashariki mwa Libya.
Wakaazi mjini Tripoli wamesema wanaogopa kutoka nje kwa sababu wana wasiwasi wanajeshi wanaounga mkono serikali huenda wakawafyatulia risasi.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema yamethibitisha kuwa watu wasiopungua mia tatu wameuwawa tangu makabiliano hayo kuanza wiki iliyopita.