Wakati taifa linakabiliwa na changamoto ya kujenga barabara za lami huku uwezo wake ukiwa mdogo kuliko mahitaji, malori aina ya Mitsubishi Fuso yanatajwa kuwa moja ya vikwazo vya kuwa na barabara bora nchini.
Kwa takribani miezi miwili sasa serikali imekuwa ikipokea malalamiko ya wamiliki wa malori makubwa wakilaumu vyombo vya usalama (trafiki), Wakala wa Barabara na hata Mamlaka ya Mapato (TRA) wanaodhibiti mizani kushindwa kukabili uharibifu wa barabara unaofanywa na Fuso.
Uharibifu huu unatokana na marekebisho yanayofanywa kwenye magari hayo kwa kuyaongezea matairi (axel) ya ziada ili yabebe mizigo mkubwa kuliko uwezo wake wa kawaida.
0 Comments