Watu wanane wakiwemo Katibu Mwenezi wa CCM Tawi la Bombambili na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Kata ya Bombambili katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, wamehukumiwa na Mahakama ya Mwanzo ya Mfaranyaki kutumikia kifungo cha nje miezi mitatu kila mmoja.
Upande wa mashtaka uliwataja washtakiwa hao kuwa ni
Ally Mussa Amanzi ambaye ni Katibu Mwenezi wa Tawi la CCM Bombambili, Hillary Mhagama Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Bombambili na Teofrida Lwena ambaye ni mke wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Merikebu Peter Haule.
Wengine ni Amina Omary,Tedy Ndumbaro,Asha Ngonyani na Juliana Albano wote wakazi wa eneo la Bombambili Manispaa ya Songea.
Akisoma Hukumu hiyo Mahakamani hapo Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Mfaranyaki Gaitan Ngasapa alisema mahakamani hapo kuwa Mahakama ime
angalia kwa makini sana mashtaka hayo ambayo yalikuwa yana mvutatano wa kisiasa .
Hakimu Ngapasa alisema ushahidi wa upande wa mashtaka uliotolewa mahakamani hapo umeonyesha wazi kwamba washtakiwa walitenda kosa kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili mwenyekiti wa Kata ya Bombambili Alfonce Haule na kumsababishia maumivu kwenye mwili wake.