Mfalme wa Swaziland, Mswati wa Tatu, ametoa wito kwa watu kujitahidi zaidi, badala ya kupinga kupunguzwa kwa ajira serikalini.Akizungumza baada ya maelfu ya watumishi wa serikali kuandamana mji mkuu hapo jana, mfalme wa Swaziland alisema, nchi haihitaji maandamano, na alitoa wito kwa wa-Swazi, kuzalisha bidhaa zaidi, kwa hivo nchi haitohitaji kuagiza karibu kila kitu kutoka nchi za nje.Msemaji wa chama kikubwa kabisa cha wafanyakazi nchini Swaziland, alisema uchumi uko katika shida kwa sababu ya mfumo wa kisiasa wa nchi, ambao alisema, unanufaisha wakubwa.
Swaziland inachagizwa kupunguza gharama za mishara ya watumishi wa serikali, ili kuweza kupata mikopo ya kimataifa.
0 Comments