KUHUSU TIBA:Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM Mkoa wa Arusha ambaye hakutaka kutaja jina lake alidai kuwa tangu alipokunywa dawa hiyo, tatizo la sukari ambalo lilikuwa likimsumbua limekwisha."Sijui kama nimepona kabisa au la, lakini sasa najisikia vizuri tofauti na mwanzo," alisema kiongozi huyo. Baadhi ya watu wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU), ambao wamepewa dawa hiyo, licha ya kudai kuwa sasa wana hali nzuri, bado hawajapima kwani wengi waliohojiwa walikuwa hawajatimiza sharti la kukaa siku saba kabla ya kupima ili wajue kama virusi vimekwisha au la.
MZIZI WA TIBA:Mchungaji Masapila alisema dawa hiyo ambayo alioteshwa na Mungu tangu mwaka 1991 na kukumbushwa mwaka 2009, inatokana na maombi na mti wa mgariga ambao ni chakula cha twiga, unaopatikana katika viunga vya Milima ya Sonjo na kupona kwa mgonjwa haraka pia kutokana na imani yake juu ya dawa hiyo ambayo dozi yake ni kikombe kimoja tu kinachonywewa hapo hapo inakotolewa.
TAMKO LA WIZARA:Blandina nyoni ambaye ni Katibu wizara ya afya amesema tayari Wizara ya Afya, imekwishatuma wataalam wake kwenda huko kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa dawa hiyo.
0 Comments