Huku mzozo wa nyuklia ukiendelea kukumba nchi ya Japan, shirika la Afya duniani limesema mionzi ya nyulikia iliyopatikana kwenye chakula imepita viwango vilivyotarajiwa.
Serikali ya Japan imewataka wakulima na wazilishaji wengine katika maeneo karibu na vinu ya nyukilia vilivyoko Fukushima kutouza mazao yao katika maeneo mengine.Huku wakikabiliana na athari zilizosababishwa na tetemo la ardhi na tusumai,pamoja na hofu iliosababishwa na mionzi ya nuclear, sasa raia wa japan wakabiliwa na tishio jingine kuhusu athari za nuclear kwenye vyakula vyao na hasa mboga.
Usafirishaji wa mboga kutoka maeneo karibu na vinu vya nuclear wa Fukushima umezuiwa baada ya uchunguzi kuonyesha kuwa mboga kutoka eneo hilo zina madini ya nuclear.
Tayari usafirishaji wa maziwa kutoka fukushima umezuiwa. Msemaji wa shirika la afya duniani magharibi mwa ukanda wa pacific Peter Cordingley anaelezea kuhusu uchunguzi huo.
'' Katika siku chache zilizopita wamgundua kuwa mboga za spinach zilizotoka maeneo yalioko kilomita 120 kutoka vinu hivyo, zilikuwa na madini ya nuclear. Sasa hio ni hatua geni na japana inalifuatilia kwa karibu. Hatua walizochukuwa ni kuzuia usafirishaji wa vyakula kutoka eneo hilo lote''
Katibu wa baraza la mawaziri Yukio Edano amewaomba watu wasiingie wasiwasi kupita kiasi kuhusu suala hilo. Amewaelezea waandishi wa habari kuwa madini hayo yaliogunduliwa kwenye mboga hayana athari yoyote kwenye afya ya binadamu.
Baada ya kuvuja kwa mionzi hiyo ya nuclear, mboga za majani na bidhaa kutoka wanayama ndio huathirikia sana. Kwa kawaida matawi ya mboga hizo ndio hupata madhara kutoka hewa yenye mionzi hiyo na nyama, maziwa na mayai huwa hatarini baada ya wanyama hao kula nyasi na matawi yaliona athari mionzi ya nuclear.
Serikali ya maerikani imesabaza madini ya potassium iodide kwa wafanyikazi wake wa wanaoishi Japana kuwa kinga na athari hiyo za mionzi ya nuclear.
0 Comments