Majeshi yanayomtii Rais anayeungwa mkono na Umoja wa Mataifa Alassane Ouattara yanaelekea kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Yamoussoukro.
Majeshi yake hivi karibuni yameteka miji kadhaa na kiongozi aliye madarakani Laurent Gbagbo ametaka mapigano yasitishwe.Bw Gbagbo amekataa kuachia madaraka licha ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa Novemba.
Mwandishi wa BBC alisema Yamoussoukro ni mji mkuu tu kwa jina, lakini kutekwa kwake kutakuwa ni ushindi wenye umuhimu mkubwa kwa majeshi yanayomwuunga mkono Ouattara.
Takriban watu 1,000,000 wamekimbia mapigano- hasa katika mji mkuu Abidjan- na karibu 462 wameuawa tangu Desemba, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Katika mji wa magharibi wa Duekoue, maelfu ya watu wamejihifadhi kwenye kanisa baada ya kukimbia mapigano wiki hii.
0 Comments