Watanzania wanaoishi nchini Belgium leo hii wamesoma kisomo cha kuhitimisha msiba uliotokea nyumbani Tanzania kwa aliyekuwa baba mlezi wa Salim Khalifan Kipanga 'Morgan'.Kisomo hicho kilifanyika nyumbani kwa Kipanga (Pichani walioketi nyuma ya viti mwenye shati la bluu mkono wa kulia ndiye Kipanga mwenyewe)wakati wakisoma dua.
kama ilivyo ada katika kila kisomo mwisho wa kisomo huwa kuna Hotuba kwa waislam kukumbushana masuala juu ya kifo,kwamba kila mwanadamu hana makazi ya kudumu hapa duniani,sasa inatubidi tujenge akhera yetu kwa mema hapahapa duniani.Pichani Shekh Habibu ambaye alikuwa akitoa mawaidha mazuri sana ambayo yalimgusa kila mmoja wetu aliyefika katika kisomo kile.mwenye shati la bluu mikono mfukoni ndiye Kipanga mwenye shughuli ya kisomo hicho.
Ndugu yetu aliyetualika kwenye kisomo bwana Salim Khalifan 'Kiapnga' baada ya dua kumalizika alitoa Sadaka kwa kila aliyejaaliwa kufika nyumbani kwake,Mungu amjaalie kwa wema wake kwa sadaka yake.
Kiongozi wa watanzania kwa upande wa wanawake waishio nchini Belgium Bidada Malika mwenye mtandio mweupe na bidada mwingine waliwawakilisha wanawake wenzao kwa kuja kutoa shukrani za dhati kwa bwana Salim khalifan Kipanga kwa shughuli nzima iliyofanyika salama nyumbani hapo.Bidada Malika amekuwa kiongozi shupavu katika kuwaweka watanzania kuwa kitu kimoja akishirikiana na Mwenyekiti wa Chama hicho bwana Ismail Hamza.
Maganga One Blogger(mwenye kofia ya bluu na miwani) hakuwa nyuma katika kusikiliza mawaidha yaliyokuwa yakitolewa kwenye Hitma hiyo.Kulia ni bwana Ahmed ambaye anaonekana akiwa ametulia akifuatilia mawaidha yaliyokuwa yakiendelea.
0 Comments