Mgombea wa kiti cha urais aliyeshindwa katika uchaguzi wa juma lililopita nchini Nigeria, Muhammadu Buhari, ametoa maelezo yake kuhusu kile anachosema kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.
Generali Buhari, alikuwa na ushahidi ulioonyesha kuwa tarakilishi za tume ya uchaguzi nchini humo, ziliwekwa programu maalum ili kumfanyia uovu katika chama chake kwenye majimbo mawili nchini humo.
Buhari amedai kuwa wafuasi wake wengi hawakuruhusiwa kupiga kura.
Hata hivyo tume ya uchaguzi nchini humo bado haijasema lolote kuhusu madai hayo.
Generali Buhari ambaye ametoka katika eneo la Kaskazini mwa Nigeriia, ambalo idadi kubwa ya watu katika eneo hilo waislamu.
Buhari alishindwa na katika uchaguzi huo na rais wa sasa wa nchi hiyo Goodluck Jonathan, anayetoka eneo la Kusi kwa nchi hiyo eneo ambalo idadi kuwa ya raia ni Wakristo.
Kumeripotiwa ghasia za baada ya uchaguzi nchini humo na shirika la msalaba mwekundu limesema takriban watu 48,000 wameyahama makaazi yao.