Nchini Burundi leo April 29 ni kumbukumbu ya mauaji ya maelfu ya raia wa kabila la wahutu waliouliwa na jeshi mwaka 1972.
Mauaji hayo yalifunikwa funikwa na tawala zilizopishana na hivi sasa baada ya mageuzi ya kidemokrasia shirika moja linakutetea haki za jamii limetaka yaliotendeka yote yawekwe wazi na haki itendeke.

Hata hivyo baadhi ya raia wa nchi hiyo wanaunga mkono juhudi za serikali ya kutenga siku ya kumbukumbu ya maujai hayo ili kuna wale wanaopinga wakisema, huenda ikasababisha uhasama kati ya jamii mbali mbali nchini humo.