Real Madrid itakutana na Barcelona katika nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuizaba Tottenham Hotspur kwa bao moja kwa sifuri kwenye uwanja wa White Hart Lane.
Bao pekee la Ronaldo liliizamisha Spurs huku Real ikisonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0.
Inter Milan nayo iliyaaga mashindano hayo baada ya kuzabwa mabao 2-1 na Schalke 04. Schalke inasonga mbele kwa jumla ya mabao 7-3.
Schalke sasa itakutana na Manchester United katika nusu fainali. United ilitinga nusu fainali baada ya kuinyuka Chelsea kwa jumla ya mabao 3-1.